Tuesday 27 October 2015

DIAMOND


                                                                                                          




KUZALIWA KWAKE.
Diamond alizaliwa tarehe 2, October mwaka 1989 katika Hospitali ya Amana Dar es salaam  na kupewa jina la  Nasibu Abdul Juma . Akiwa na umri mdogo wazazi wake walitengana na baba yake kumuacha bila msaada wowote  na ikabidi wahamie Tandale Magharibi kwa bibi  yake mzaa mama, na hapo ndipo yakawa makazi yao.. Historia yake ni ya kusikitisha kama alivyoelezea kwenye wimbo wa binadamu wabaya.
ELIMU YAKE.
Mnamo mwaka 1995  alianza kupata elimu ya Nursery katika shule ya Chakula Bora iliyopo  Tandale Uzuri hadi alipomaliza na kujiunga na Elimu ya Msingi yaani  (Primary School) mwaka 1996 katika shule ya msingi Tandale magharibi  iliyopo jijin Dar-es-salaam na kuhitimu shule ya Msingi mwaka 2002. Baadae akahitimu elimu yake ya Secondary mwaka 2006.

SAFARI YAKE YA MUSIKI NA MAFANIKIO YAKE.
Akiwa darasa la tano  diamond alionekana kuanza kupenda sana muziki, hivyo alianza kunakili  baadhi ya nyimbo na kukariri nyimbo za wasanii waliokuwa makihri ndani na nje ya  nchi kwa kipindi hicho na kuwa anaimba katika sehemu tofautitofauti.Mara nyingi mama yake alikuwa akimnunulia kanda za album  za wasanii tofauti  waliokuwa makihiri kipindi hicho na hata kumuandikia baadhi ya nyimbo za  wasanii hao ili mwanae aweze kuzishika na kuimba kirahisi, na wakati  mwingine hata kumpeleka katika matamasha tofautitofauti ya vipaji vya watoto  ili mwanae apate nafasi ya kuimba, kitu ambacho baadhi ya ndugu wa  familia waliona ni kama kumpotosha na kumuharibu mtoto huyo badala ya  kumuhimiza kimasomo. Kiukweli hali ya maisha yao ilikuwa ni ngumu saana, maana mama Diamond hakuwa hana mradi wowote ya kumuingizia kipato, hivyo  ilibidi atumie kias kidogo anachokipata toka kwa kodi ya vyumba viwili  alivyopewa na Mama yake yaani bibi yake diamond na vibiashara vyake  vidogovidogo vya mikopo kwa kumsomeshea na kumlea diamond. Hali  yao ya Kimaisha ilikuwa ni ngumu sana, hivyo iliwaradhimu wote kuhamia  katika chumba cha bibi huyo ili kupangisha vyumba vile viwili alivyopewa
mama diamond
Ilipofika mwaka 2003 baada ya Diamond  kutaka  kuanza masomo ya Secondary   mama yake alimwambia aachane na muziki kabisa na azingatie na Masomo ili aweze kupata elimu itayomsaidia hata kwa muziki wake baadae kwa maana asingeweza kushika vitu viwili  kwa pamoja muda huo. Akiwa secondary diamond aliendelea kufanya muziki  kisirisiri bila mama yake kujua na kufikia mwaka 2004 taratibu akaanza  kujifunza kuandika nyimbo zake mwenyewe. 2006 mwaka 2007 alijikita rasmi katkia sughuri za  muziki ili kujaribu kutimiza ndoto zake.kiukweli haikuwa ni safari  rahisi kama alivyotegemea hadi kupelekea mda kuanza kutafuta vibarua  toafauti tofauti ili mradi aweze kupata riziki na kuepuka hali ya  kushinda nyumbani, ikiwemo kuuza mitumba, petrol station, kupiga picha,kazi za viwandani hata wakati mwingine kuingia kwenye  makundi ya kucheza kamali za mitaani ili aweze kupata pesa ya kuingia  studio kurecord lakini bila kufanikiwa, kiukweli ikabidi imradhimu kuuza pete ya Dhahabu ambayo alipewa na mama yake mzazi aivae na kumdanganya kuwa ameipoteza na ndipo hapo alipofanikiwa  kuingia studio kurecord nyimbo ya kwanza iitwayo ‘TOKA MWANZO’ kutokana na kutokuwa na mazoea ya kurecord hakuweza kutengeneza nyimbo ambayo ilivuma sana lakini wimbo ule ulianza kumpa jina kutokana na watu wengi walishangazwa jinsi alivyoingia kwa mara ya kwanza studio na kuweza  kutengeneza wimbo kama mtu ambae ni mzoefu, hivyo iliwafanya kuamini  kuwa akipata nafasi ya kurecord mara kadhaa angeweza kufanya kitu  kikubwa..Wimbo ule ulimfanya aweze kukutana na Chizo mapene ambae  alijitolea kumsimamia kazi zake na wakaanza kurecord album lakini bahati mbaya wakiwa katikati ya kurekodi album hiyo anayemsaidia alipata  matatizo ya kifedha na hakuweza tena kumsaidia hivyo ilimbidi  Diamond aanze tena upya kuzunguka katika studio tofauti kuomba  kuingia mkataba kwenye record label lakini kote hakuweza kufanikiwa, wote walimwambia bado hajui kuimba na kutotaka kumsikiliza kabisa.Kilikuwa ni kipindi kigumu sana maana hata yule mpenzi wake ambae alikuwa nae alimuacha kwakua alikuwa ameshachoshwa na ndoto hewa ambazo  alikuwa akiziota kila siku diamond kuwa ipo siku atafanikiwa kimuziki na kuwa mwanamuziki mkubwa na wao kuish maisha









mazuri, kitu ambacho kilimchanganya na kumuumiza sana Diamond.Mwaka 2009,  Diamond alikutana na Bwana Msafiri Peter  maarufu  kama Papaa Misifa ambae alikubali kumsaidia kimuziki na kurecord wimbo wa kwanza ulioenda kwa jina la “KAMWAMBIE”, ni wimbo  ambao Diamond aliimba  kwa uchungu  huku akimuimbia mpenzi wake huyo aliyemuacha (Sarah Sadiki) kuelezea kiasi  gani  aliumia kwa yeye kumuacha kwake, na hapo ndipo taratiibu nyota yake
ikaanza kung’aa na wimbo huo kukua siku hadi siku.Maisha yake yakabadilika  na Diamond kuweza  kununua gari  aina ya Toyota Celica. Tarehe  14/02/2010 Diamond aliachia  album yake ya kwanza iliyokuwa na nyimbo 10 ambazo ni kamwambie  , Mbagala  , Nitarejea  , Nalia na mengiBinadamu  , Nakupa  , Usisahau  , Uko tayari  , Wakunesanesa  , Toka mwanzo  na Jisachi. Mnamo tarehe 04 mwezi wa  4 mwaka 2010 , Diamond aliandika record ya kuwa msanii wa kwanza Tanzania kushinda tunzo tatu za Tanzania Kili Music Awards kwa pamoja
ambazo ni: Msanii bora Chipukizi, Wimbo bora wa Mwaka (KAMWAMBIE) na  Wimbo bora wa R&B(KAMWAMBIE), tunzo ambazo zilimfanya achaguliwe  kuwa balozi wa Malaria nchini Tanzania.Baada ya kuachia wimbo wake wa  pili  unaoitwa Mbagala,  Diamond alichaguliwa na Rais wa  jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr Jakaya Mrisho kikwete kuwa  mtumbuizaji katika safari  nzima ya Kampeni yake.  Tarehe 02 -10 -2010 alipa  safari ya kwanza kwenda England mjini LONDON,MILTON KEYNES, na COVENTRY.  Baada ya  kuachia  wimbo wake wa tatu mwaka 2011  , Diamond alishinda tuzo ya
Nzumari  Award nchini Kenya akiwa kama Msanii bora wa Kiume toka  Tanzania.  Diamond aliachia nyimbo yake ya nne na kuweka record ya kuwa msanii wa kwanza na pekee kujaza Club Maisha hadi watu  kushindwa kuingia na hata wengine kuzimia baada kutokupata hewa ya kutosha kutokna na wingi ujaaji huo.Mwaka mpya wa 2012, tarehe 1 -1- 2012 , Diamond Platnumz aliachia album yake ya pili  na kuweka record ya kuwa msanii wa kwanza Tanzania kuuza zaidi ya nakala 1200,000 . Mwanzoni mwa mwaka 2012 Diamond aliweka record kuwa msanii wa kwanza Tanzania kufanya show ya USHIRIKIANO iliyoitwa ” Diamond forever” iliyofanyika Mlimani City  kwa kiinglio  cha shilingi elf hamsini 50,000  za kitanzania akiwa pekeake na  kuuza ticket   zaidi ya 1,500.Mnamo mwezi wa 5 mwaka 2012 , Diamond Platnumz  aliweka record ya kuwa msanii wa kwanza kufanya show na kujaza zaidi ya watu 10’000 kwa kiingilio cha 20,000 katika kiwanja cha Darlive  huku akishuka na Helicopter kwenye Stage. Mwaka huohuo  Diamond alifanya ziara yake ya Europe ikiwemo Italy, Holland, Sweden ,  Greece na kumalizia ziara yake ya arabuni nchini Masqat  Oman.Mwishoni mwa mwaka 2012 ulikua mzuri kwa Diamond Platnumz kwani aliweza kuachia nyimbo mbili kwa mpigo za “Nataka kulewa ” na “Kesho ”.Mwezi wa kumi na mbili mwaka  2012 diamond alitajwa kuwa ni msanii wa kwanza anaelipwa Pesa nyingi kwenye Show toka Tanzania Mwanzoni mwa mwaka 2013 , Diamond  Platnumz alichaguliwa na Cocacola kuwa Balozi wa Kinywaji Cha Cocacola, na  kufuatiwa na ziara yake ya East Africa na ikiwemo Burundi  , Congo na Kenya n.k. na kuweka record ya kuwa msanii wa kwanza East Africa kuwezakupiga show pekeake kwenye uwanja na kujaza zaidi ya watu 30,000… mnamo  June 2013 Diamond alishinda tuzo mbili  za Tanzania Kili Music  Award akiwa kama   Msanii bora wa kiume Bongoflavour na Msanii bora  wa kiume kwa wanamziki wote Tanzania.Mwezi wa saba mwaka 2013 , Diamond  aliachia nyimbo yake yake iliyokwenda kwa jina la Number One ambayo  aliifanyia Video Capetown South Africa chini ya kampuni ya Ogopa  Videos  na kuweka record ya kuwa msanii wa kwanza kulaunch video bila  kiingilio katika Hotel ya SERENA na kuwaalika,  na  viongozi toka sehemu tofauti tofauti. katika chakula cha mchana hiyo akamzawadia Gari moja ya nguri mkubwa katika mziki wa Tanzania , Marehemu  Mwidini Gurumo.mwezi 10 mwaka 2013 .Diamond aliifanya Collabo na msanii toka Nigeria  Davido katika wimbo wake wa Number one kama Remix  kutoa video ya wimbo huo  na Kampuni ya Capital Dreams iliyo chini ya Director  Clarence Peter. Nyimbo hii ilimtambulisha Diamond Platnumz nchini Nigeria na barani Africa kiujumla na kumuwezesha kupata nominations mbalimbali kwenye tuzo za kimataifa ikiwemo , MTV MAMA awards ambayo aliperform nyimbo hii live na Davido, BET Awards na tuzo zinazotegemea kufanyika za AFRIMAMA , MTV Europe , Channel O awards na awards nyingine kutoka nchi mbalimbali.Tarehe 7 - 7 - 2014 , wakati Diamond akisherekea Birthday ya mama yake alimzawadia mama yake gari pamoja na kuachia video mbili za mdogomdogo aliyoifanyia nchini Uingereza na BumBum aliyomshirikisha Iyanya kutoka Nigeria aliifanyia Afrika Kusini. Video hizi  kwa pamoja zilimgarimu Diamond dola 78,000 za kimarekani . Hivi Sasa nyimbo hizi ndio habari ya mjini na ni kitu kisichofikisha kwamba nyimbo hizi zitaendelea kumbeba Diamond hadi mwaka 2014 unaisha.Huyu ndio Diamond Platnumz, mtoto wa Tandale aliyoweza kutumia kipaji chake cha kuimba vizuri, aliyoweza kukabiliana na changamoto mbalimbali za maisha ,maisha yake ni fundisho kwa vijana kibao mjini wanaohangaika kutoka kimaisha.



1 comment:

  1. The article is really good, permission to comment here admin Pesona mata

    ReplyDelete