Friday 30 October 2015


 
Wema Sepetu alizaliwa tarehe 28, September 1988, ni mtoto wa mwisho kati ya mabinti wanne wa Mzee Sepetu.
Wema hakufikiria kama atakuja kuwa mmoja kati ya ma-star wakubwa hapa nchini hadi nchi za nje mpaka siku mmoja alipo kuwa kwenye matembezi yake Slypway Masaki alikutana na dada Mange Kimambi na kushawishiwa ashiriki mashindano ya Miss Tanzania 2006...

 Wema Sepetu aliibuka kidedea na kuwagalagaza Jokate Kidoti Mwegelo na Lisa Jensen

MAHUSIANO

Kabla ya kuwa miss Tanzania alikuwa na mpenzi lakini hawakudumu maana aliposhikilia taji alikuwa bize jambo lililomfanya akose muda wa kutulia na mpenzi  wake lakini muda mchache akakutana na Marehemu Kanumba na kuanza uhusiano . Kanumba ndiye aliye gundua kipaji cha Wema na ndiyo aliye muibua katika sanaa ya kuigiza.

Uhusiano baina ya Kanumba na Wema ulikwenda vizuri sana na nyota zao zote zikang'aa sana  hii ni kutokana walishirikiana katika movies zao na kufanya  kuzidisha umaarufu mara dufu.


 
 Pichani ni Wema na mpenzi wake Steven Kanumba enzi za uhai wake Kanumba .

 
Mahusiano ya Wema na marehemu Kanumba yalivunjika baada ya ugomvi uliotokea kati yako na Wema  kuamishia mapenzi  Jumbe.


Wema  akiwa na mpenziwake wa zamani Jumbe 

Mahusiano ya Wema  Sepetu na Jumbe pia hayakudumu sana na Wema  akajikuta  akiangukia mikononi mwa Chalz Baba.Kwa  bahati mbaya uhusiano huu pia haukudumu.


Baada ya kutulia kipindi bila kuwa kwenye mahusiano,Wema  akajikuta akiingia kwenye mahusiano kwa mara nyingine na mkali wa miondoko ya  R&B Tanzania na kwa Africa pia  “Diamond platinum”ambaye uhusiano wao ulikatishwa na skendo mbali mbali zilizokuwa zinatokea juu yao.
Picha ya Diamond na Wema

MAFANIKIO YAKE

Wema sepetu anamiliki kipindi cha television kinachojulikana kwa jina  la  "IN MY SHOES".na pia anajishughuisha na maswala ya mitindo ya mavazi.Pia anajishughulisha na  sanaa ya filamu.Kutokana na shughuli zake amekuwa ni mwanamke mwenye umaarufu mkubwa na mwenye hali  nzuri ya kiuchumi katika jamii.






2 comments:

  1. youtube - vipvideogames.com, youtube vipvideogames.com
    youtube - vipvideogames.com The following video is shown in 3 different ways. youtube converter 1) Play this Video Game and 2) Enjoy The Best and Worst Game of The Month.

    ReplyDelete