Tuesday 27 October 2015

MR BLUE.


                                                                                                     
Khery Sameer Rajab au MR.BLUE kama tulivomzoea,amezaliwa tarehe14-4-1987.Ni msanii wa muziki wa R&B na Bongo Flava  kutoka nchiniTanzania . Alifanikiwa kujizolea umaarufu mkubwa huku akipendwa na wapenzi na mashabiki, mara tu baada ya kuingia katika fani ya muziki na wimbo wake 'Mr Blue'. Ambapo baadaye ikaja kuwa kama ndiyo jina lake la kisanii.
Mr Blue alikuwa gumzo na wimbo 'Mr Blue' kabla ya kuja kupata umaarufu zaidi na wimbo wake wa 'Mapozi', ambao ndiyo uliomzidishia kupendwa kutokana na mpangilio wa mashairi na sauti aliyotumia pamoja na maujanja ya ala ya muziki wenyewe.

MR BLUE ni mtoto wa tatu kati ya wanne kwa kuzaliwa katika familia ya mzee Sameer Alhaji Alhad Ally mwenye asili ya Ki-Sudan.
Elimu yake ya msingi aliipata katika shule ya Gerezani ambako alihitimu mwaka 1999, lakini hakuweza kumaliza elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari ya Dar es Salaam, ambako aliishia kidato cha pili mwaka 2004, hii ni kutokanana changamoto zilizokuwa zikimkabili.Mahitaji ya kifedha yalikuwa makubwa na ulifika wakati alilazimika aidha kuchagua muziki au shule, kwa kuwa muziki ulikuwa ukitatua tatizo la kifedha, basi hakuwa na budi kuchagua muziki.MR BLUE  alikuwa anaeleza kuwa bado ana mpango wa kujiendeleza kielimu alipokuwa anahojiwa na vipindi mbalimbali vya mahojiano kuhusiana na maoni yake juu ya kujiendeleza kielimu.

MR BLUE alianza kujihusisha na masuala ya muziki mwaka 1999, na kilicho sababisha ajiingize katika fani hiyo ni kaka zake waaliojulikana kwa majina ya The Boy Stain na Obrey, ambao nao walikuwa wakijihusisha na suala zima la muziki.
Lakini hakuanza kuimba moja kwa moja, bali alikuwa akifuatilia tu jinsi gani muziki unavyokua, na mwaka 2001 ndipo nilipojiingiza zaidi kwa kuanza kuimba katika sherehe mbalimbali za 'Macamp.
"Mwaka 2003 kuelekea 2004 ndipo alipotoka na wimbo wake wa 'Mr Blue' ambao ndiyo ulioanza kumapatia umaarufu.
Wakati akitamba na kibao chake hicho, lakini hakutaka mashabiki wamsahau mapema, hivyo aliamua kutoa kibao kingine kilichokwenda kwa jina la 'Mapozi', ambacho kilimtangaza na kupiga hatua kupitia nyimbo hizo,ambaye albamu yake ya kwanza ilikwenda kwa jina la 'MR BLUE' na ya pili ni 'YOTE KHERI'.

MR BLUE anawashukuru mama yake mzazi Halima Rajab ambaye kwa saizi ametangulia mbele ya haki na baba yake Sameer Alhaj Alhad Ally kwa kumruhusu kujikita katika muziki.

MR BLUE aliwahi kuwa na mahusiano na msanii mwenzake anayejulikana kama Naj anayeishi jijini London. uhusiano huo uliisha kitambo kidogo na sasa MR BLUE ana mke ambaye wamebahatika kupata nae mtoto mmoja.

No comments:

Post a Comment