Friday 30 October 2015

LAD JAYDEE





Kuzaliwa kwake

Judith Wambura au Lady Jaydee alizaliwa  mkoani Shinyanga mnamo tarehe 15 Juni,1979 na wazazi wake Martha na Lameck Isambua Mbibo.. Baada ya kumaliza shule, Lady Jaydee aliwahi kufanya kazi Clouds FM kabla ya kuamua kujiingiza kwenye masuala ya muziki hapo mnamo miaka ya 2000

Safari yake ya musiki

Alianza kuimba akiwa na umri wa miaka saba. Alianzia kuimba kanisani kama ilivyo kwa wasanii wengi.Alianza kujibebea heshima katika medani ya muziki kunako mwaka wa 2000 baada ya kutoa albamu yake ya kwanza iliyokwenda kwa jina la "Machozi" na kutoa single kadhaa kutoka katika albamu hiyo na kumfanya kuwa mwanamama wa kwanza katika bongo flava kwa kutumia gharama kubwa ya ujenzi wa albamu katika historia ya muziki wa kizazi kipya.
Lady Jay Dee ni msanii mwenye kumiliki studio yake mwenyewe ya kurekodia. Studio inakwenda kwa jina la Jag Records.
Jay Dee, alishawahi kuchaguliwa kuwa Mwanamuziki Bora wa Kike wa Tanzania kwa muziki wa 
R&B mnamo 2002, na kutumbuiza katika kora All Africa Designers Competition, na kutuzwa "Albamu Bora ya R&B" katika Tuzo za musiki Tanzania kunako tar. 6 mwezi wa nane. Kunako mwezi wa Julai 2005, ameshinda tuzo ya "video bora ya msanii wa kike kwa Afrika Kusini"

Baadhi ya albamu za Jaydee ni;

·         Machozi (2000)
·         Binti (2003)
·         Moto (2005)
·         Shukrani (2007) 


**"Lady jy dee amewahibahatika kuolewa na mmojawa watangazaji wa clouse media Gardner G Abashi."

**Lady Jay Dee amepata mafanikio makubwa kutokana na kupewa mchango mkubwa toka kwa wanafamilia wake. 






No comments:

Post a Comment